Shirika la Safe Space for Children and Young Women Tanzania limefanikiwa kuendesha mafunzo ya stadi za maisha na ujasirimali kwa wasichana 15 walio chini ya umri wa miaka 24 katika Wilaya Ubungo. Lengo la mafunzo haya ni kuendeleza juhudi za kuwakwamua wasichana walio nje ya shule kiuchumi ili waweze kuendesha maisha yao wao wenyewe katika jamii.