Katika kuunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha kila mtoto anapata elimu iliyo bora,, Shiraka la @safespacetanzania Kupitia mradi wa uwezeshaji wa mazingira salama ya kujifunzia wanafunzi katika kata ya Katunguru iliyoko wilaya Sengerema Mkoani Mwanza, limefanikiwa kukabidhi vitabu 850, madaftari 2000 pamoja na vifaa vingine vya kijifunzia Watoto katika shule ya msingi Chamabanda. Ufadhili huo unawanufaisha watoto 964 katika shule hiyo.
